Wednesday, October 28, 2009

UMUHIMU WA INTERNET KWA WAANDISHI WA HABARI

Na Wilson Elisha, Mwazna
Umuhimu wa Internet kwa waandishi wa habari

Utumiaji wa Internet kwa waandishi wa habari katika shughuli zao za kila siku ni njia mojawapo inayowarahisishia kufanya kazi zao .
Kazi hizo zimekuwa ni chachu na changamoto kubwa miongoni mwa jamii ya Kitanzania ambayo imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu sana vyombo vya habari.
Licha ya wananachi wengi kutojua umuhimu wa kutumia matandao kutafuta habari na kuzisoma kwa njia ya mtandao bado wanaamini kuwa kazi inayofanywa na waandishi wa habari kupitia vyombo vyao vya habari ni nzuri na za uhakika.
Mafunzo ya Internet kwa waandishi wa habari yamekuja kwa muda muafaka ambapo hasa ukizingatia kwamba hivi sasa ulimwengu niwa sayansi na teknolojia unahitaji kufahamu namna ya kutumia njia ya mawasiliano iliyorahisi tofauti na miaka iliyopita.
Katika siku ya pili ya mafunzo ya Internet yanayotolewa na mkufunzi Bwana Peik Johansson, kutoka Finland, kwa waandishi wa habari wanaoshiriki, kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni Shinyanga, Mara, Kagera na Mwanza wameweza kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo utumiaji wa Internet.
Katika mafunzo hayo washiriki wamefanikiwa kujifunza namna ya kutafuta mambo mbalimbali kwa kutumia njia ya tovoti (wavuti) au mtandao.
Mitandao mingi imefunguliwa na watu mbalimbali ambao wanaamini kuwa kile kilichoandikwa katika mitandao hiyo ni wazi kuwa kinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine kutambua ulimwengu unavyokwenda hivi sasa sanjari nay ale matukio yaliyopita.
Kwa upande wa matukio yaliyopita hii ni njia nzuri ya kukifahamisha kizazi kilichopo na kile kijacho juu ya matukio hayo ambayo ni historia itakayosaidia kutambua yale yaliyopita mfano vita vya Iraq na Marekani.
Mfano halisi ni Bw. Alexa ambaye alifungua matandao wake na kuweka matukio muhimu yanayohusu ulimwengu, ambaye katika website 500 inashika nafasi ya kwanza katika website zilizofunguliwa huku Bw. John Naugthon website yake ikiwa imeweza kubadili mambo mbalimbali.
Kwa upande wa mtandao wa Bw. eBay wa www.ebay.com kwa kipindi cha mwaka 2009 umeweza kusajili watu wapatao milioni miamoja wanaotumia mtandao huo . Pia katika mtandao huo unaweza kuuza kufanya makubaliano na kununua vitu kadhaa kutoka kwa watu mbalimbali duniani.

No comments:

Post a Comment