Tuesday, October 27, 2009

mafunzo ya internet kwa waandishi wa habari

Matumizi ya Internet duniani yameleta mabadiliko kwa jamii

Kutokana na mafunzo haya ya Internet, ambayo yataendeshwa kwa siku tano, yataleta changamoto kubwa miongoni mwa washiriki.
Katika siku ya kwanza tumeweza kujifunza namna Internet inavyoweza kubadilisha jamii katika mawasiliano ya haraka naya uhakika hasa ukizingatia ulimwengu tulionao ni wa sayansi na Teknolojia.
Aidha matumizi ya Internet kwa kiwango cha dunia licha ya matumizi hayo kuzidi kuenea katika nchi nyingi duniani, takwimu zikionyesha kuwa katika nchi bora 20, China ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi wa Internet ikifuatiwa na United States of America,.
Kwa upande wa bara la Afrika katika nchi 10 bora kwa watumiaji wa Internet ,Egypt ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wanaofikia asilimia 12.6 na inafuatiwa kwa ukaribu na Nigeria yenye watumiaji wanaofikia asilimia 11.0 huku nchi ya Zimabwe ikiwa niya 10 kwa kuwa na watumiaji wanaofikia asilimia 1.4.
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ya Internet duniani, hivi sasa mtu yeyote anayetaka kusafirianaweza kufanya booking ya ndege katika nchi anayotaka kusafiri sanjari na kujua bei ya tiketi kutoka kituo kimoja kwenda kingine, mfano Dar es Salaam To Bujumbula, Entebe To Nairobi.
Pia tumeweza kujifunza na kutambua historia ya matumizi ya Internet yalivyoanza katika kipindi cha mwaka 1957 katika Muungano wanchi za Kisoviet kwa njia ya Sputrik Satellite.
Watu mbalimbali duniani wanawasiliana kwa kutumia njia ya E- mail ambayo imerahisisha mawasiliano hata waandishi wengi wanaotumia Internet kwa kutuma habari kwa vyombo vyao tofauti na zamani ambapo walikuwa wakitumia njia yasimu au barua.
Hadi kufikia mwisho wa mafunzo hayo ninauhakika nitakuwa nimepata elimu ambayo itaweza kunisaidia katika suala zima la utumiaji wa Internet sanjari na kuitumia elimu hiyo kwa manufaa ya watu wengine ambao hawakuweza kupata nafasi ya kuhudhuria .

No comments:

Post a Comment