Wednesday, October 28, 2009

MISA -TANZANIA NA ELIMU YA INTERNET KWA WAANDISHI

Na Wilson Elisha, Mwanza oktoba 28,2009 day three
MISA- TANZANIA NA ELIMU YA INTERNET KWA WAANDISHI

Kuendelea kutolewa kwa mafunzo ya Internet kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika -Tanzania (MISA- TANZANIA), kuwapa elimu zaidi ya namna ya kutumia mtandao (Tovuti), web site.
Mafunzo hayo yanayotolewa na mkufunzi kutoka nchini Finland Bw. Piek Johansson , yamekuwa ya kifundishwa kwa njia ya vitendo na nadhalia na yameingia katika siku yake ya tatu ambapo washiriki wamekuwa wakifuatilia kwa umakini na uhakika.
Katika siku ya tatu washiriki walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kupata habari za kimataifa (INTERNATIONAL NEWS) kutoka nchi yoyote duniani , kwa njia ya mtandao sanjari na kujua historia ya nchi husika.
Aidha ilibainisha kwamba Internet ni chombo muhimu kwa taaluma ya waandishi wa habari ambao ni kiungo kikubwa katika nchi nyingi duniani ambapo wananchi hutegemea kupata habari zinazotafutwa na waandishi hao.
Aliongeza kuwa utamaduni wa waandishi wa habari kupata habari , unatokana na kuona, kusikia, chanzo cha mtu moja moja, watu, mawasiliano, press releases pamoja na kutoka vyombo vingine vya habari kulingana na umuhimu wa habari husika.
“Badala ya kununua magazeti mtu/watu wanaweza kusikiliza kituo cha Radio na hivyo kupata habari kwa njia hiyo au vyombo vingine ambavyo vinatoa habari,”alisema Mkufunzi
Kwa upande wa utafutaji wa habari katika vyombo vingine (other media), mkufunzi huyo alisema kuwa unaweza kupata habari kwa kuangalia mtandao (Tovuti) ambai ni muhimu na alitoa mfano wa magazeti kadhaa kutoka Barani Afrika, daily National, Habari leo, Tanzania Daima, Mwananchi, na IPP median.
Pia alisema kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia hiyo ya Internet, waandishi wa habari wanaouwezo wa kutafuta habari nyingi kupitia mtandao (website) Bunge website, Jamii forums(Mwanakijiji) na nyinginezo.
“Kwa kupitia mtandao hivi sasa unaweza kupata historia ya Rais wan chi yoyote duniani na nmana nchi hiyo inavyoendelea katika masuala mbalimbali yakiwemo yale ya kisiasa, kiuchumi, mazingira, michezo na utamadunu wan chi husika.
Mafunzo hayo yalifanyika katika chuo cha Benk kuu (BOT) kilichoko Jijini Mwanza na yaliwashirikisha waandishi wa habari wapatao 20 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na yalidhaminiwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika- Tanzania ( MISA – TANZANIA).

No comments:

Post a Comment