Friday, October 30, 2009

Albino na simu za kukabiliana na mauaji

Tuesday, January 06, 2009
Albino Tanzania kupewa simu za kukabiliana na mauaji

"Hatimaye jamii ya albino inatarajia kupewa simu za mkononi ili kuwawezesha kuwasiliana na polisi kwa haraka ikiwa ni mojawapo ya kutafuta njia muafaka za kupambana na mauaji ya albino yanayochochewa na imani potofu za uchawi na ushirikina.

Kamanda wa polisi mheshimiwa Suleiman Kova amesema kuwa simu takribani 350 zimekusanywa toka kwa watu mbalimbali waliojitolea katika zoezi hilo na kwamba simu hizo zitagawiwa kwa albino na familia zao kwa lengo la kuimarisha usalama wa wanajamii hao.
Hadi sasa, idadi ya watu waliopoteza uhai kutokana tu na rangi ya ngozi yao ni 35.
Siku kadhaa nimewahi kuandika kuhusiana na suala la ualbino na Tanzania.

Nadhani inaweza ikawa ni wazo zuri lakini nachelea kufikiri kuwa inaweza ikawa hatari zaidi kwa albino na familia zao kwani watu waovu wakishafahamu kuwa wanajamii hawa wana simu za bure, inawezekana kabisa hiyo ikawa ndiyo sababu ya kuwashambulia ili kujipatia simu za bure, na hivyo, badala ya salama ikawa karaha.

Suala jingine pia ni kuhusu kuihudumia simu yenyewe kwani simu ili iweze kufanikisha lengo lake la mawasiliano, itahitaji kupewa nguvu kwa kuchaji na kuwa na muda wa hewani. Sifahamu kwa watu wanaoishi vijijini ambapo nishati ya umeme ni tatizo, watawezaje kumudu kuziweka simu zao na nguvu ya kutosha kumudu mawasiliano.

Pia, ikiwa wanaopewa simu hizi hawatakuwa na kipato cha kuwawezesha kununua vocha za muda wa hewani, huu utakuwa mzigo badala ya msaada, labda iwe kwamba makampuni ya simu za mkononi yameruhusu baadhi ya namba zao zitumike bure kwa ajili ya mawasiliano haya (kama ilivyokuwa kwenye simu za bure za HIV/AIDS Helpline ya TAYOA).

Nijirudi mwenyewe na kusema kuwa, kwa kila jambo, lazima kuwe na pa kuanzia, hivyo basi ni vyema tujaribu na tuone ikiwa tunafanikiwa katika hili, la, isipowezekana na kama hasara itaonekana mapema, basi zoezi hili lisitishwe na tutunge tena njia nyingine ya kuwalinda wanajamii wetu.

Ni vigumu sana kwa binadamu kupata suluhisho la moja kwa moja kwa matatizo yake ndiyo maana nakubali kuwa, tujaribu njia hii na tuone ikiwa itafanikiwa ama la.
label: Habari/News |" NB. Hii ni taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa wavuti.com

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limetamba kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, jeshi hilo limefanikiwa kutekeleza mikakati yake na kufanikiwa kudhibiti mauaji mapya, hivyo kurejesha matumaini.

Rwambow akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wa Afrika Kusini, ofisini kwake mwishoni mwa wiki, alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi lake.

Alisema watuhumiwa zaidi ya 30 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani wakiwemo waganga wa jadi wanaoendekeza upigaji wa ramli, na waganga wawili wameshahukumiwa kifungo.

Wakati Jeshi la Polisi likidai kupata mafanikio mkoani Mwanza, leo gazeti hili lina habari kuhusu mauaji ya kikatili yaliyotokea mkoani Shinyanga dhidi ya mwanafunzi Matatizo Dunia (13) mwenye ulemavu huo wa ngozi (Albino).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Magesa Mulongo, mwanafunzi huyo aliuwawa kikatili na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake, wakati akitoka kutazama video yeye na vijana wenzake watano ambao hivi sasa wanashikiliwa na polisi.

Tunasita kutoa pongezi zetu kwa mafanikio ambayo Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linadai limeyapata katika mapambano dhidi ya mauaji ya Albino, kwani tunaamini mapema mno kuzungumzia mafanikio katika kipindi hiki.

Wakati mkoani Mwanza taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya maalbino 11 wameuawa kikatili,wawili wamepotea na makaburi matano kufukuliwa, bado hakuna sensa rasmi iliyofanywa ili kutambua idadi ya maalbino waliokuwemo na waliopo hivi sasa ndani ya mkoa huo.

Tunahofu kuwa, kwa kutokuwa na takwimu sahihi na rasmi, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linaweza kuwa linajisifu kwa mafanikio hewa , kwa kudhani kuwa mauaji yamepungua kumbe kuna wengine wanaopoteza maisha yao pasipo kujua kama walikuwepo.

Tukizingatia mauaji ya kikatili yaliyotokea Shinyanga –mkoa ulio jirani na mkoa wa Mwanza, tunazidi kuwa na mashaka na mafanikio ambayo Kamanda Rwambow ameyataja kuyapata mkoani Mwanza.

Tungependa tueleweke vizuri hapa, kwamba tunathamini jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza lakini hatuungi mkono jitihada hizo kuitwa mafanikio, ni mapema mno.

Jeshi la Polisi bado lina changamoto kubwa ya kuwakamata wauaji halisi wa albino na kudhibiti mauaji hayo, kwani uzoefu unaonesha kuwa mauaji mengi ya albino hutokea katika mazingira yanayoashiria kutokuwepo kwa usalama maalum kwa ajili ya maalbino.

Tunalishauri Jeshi la Polisi, likishirikiana na wadau mbalimbali nchini wakiwemo wananchi, lianzishe ulinzi maalum na endelevu kwa ajili ya maalbino, huku vyombo vingine vinavyohusika vikitimiza wajibu wa kutoa elimu dhidi ya wale wote wenye imani potofu kuhusu albino.

Mafanikio yoyote hupimwa kwa kuzingatia ni katika kipindi gani mafanikio hayo yamepatikana, kwa muda huu tulionao ni dhahiri kuwa ni mapema mno kwa Jeshi la Polisi kujisifia kuwa linapambana vema na wauaji wa albino"
.Nukuu hii inatokana na tahariri ya gazeti la Tanzania Daima la Desemba 2008JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limetamba kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, jeshi hilo limefanikiwa kutekeleza mikakati yake na kufanikiwa kudhibiti mauaji mapya, hivyo kurejesha matumaini.

Rwambow akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wa Afrika Kusini, ofisini kwake mwishoni mwa wiki, alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi lake.

Alisema watuhumiwa zaidi ya 30 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani wakiwemo waganga wa jadi wanaoendekeza upigaji wa ramli, na waganga wawili wameshahukumiwa kifungo.

Wakati Jeshi la Polisi likidai kupata mafanikio mkoani Mwanza, leo gazeti hili lina habari kuhusu mauaji ya kikatili yaliyotokea mkoani Shinyanga dhidi ya mwanafunzi Matatizo Dunia (13) mwenye ulemavu huo wa ngozi (Albino).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Magesa Mulongo, mwanafunzi huyo aliuwawa kikatili na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake, wakati akitoka kutazama video yeye na vijana wenzake watano ambao hivi sasa wanashikiliwa na polisi.

Tunasita kutoa pongezi zetu kwa mafanikio ambayo Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linadai limeyapata katika mapambano dhidi ya mauaji ya Albino, kwani tunaamini mapema mno kuzungumzia mafanikio katika kipindi hiki.

Wakati mkoani Mwanza taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya maalbino 11 wameuawa kikatili,wawili wamepotea na makaburi matano kufukuliwa, bado hakuna sensa rasmi iliyofanywa ili kutambua idadi ya maalbino waliokuwemo na waliopo hivi sasa ndani ya mkoa huo.

Tunahofu kuwa, kwa kutokuwa na takwimu sahihi na rasmi, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linaweza kuwa linajisifu kwa mafanikio hewa , kwa kudhani kuwa mauaji yamepungua kumbe kuna wengine wanaopoteza maisha yao pasipo kujua kama walikuwepo.

Tukizingatia mauaji ya kikatili yaliyotokea Shinyanga –mkoa ulio jirani na mkoa wa Mwanza, tunazidi kuwa na mashaka na mafanikio ambayo Kamanda Rwambow ameyataja kuyapata mkoani Mwanza.

Tungependa tueleweke vizuri hapa, kwamba tunathamini jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza lakini hatuungi mkono jitihada hizo kuitwa mafanikio, ni mapema mno.

Jeshi la Polisi bado lina changamoto kubwa ya kuwakamata wauaji halisi wa albino na kudhibiti mauaji hayo, kwani uzoefu unaonesha kuwa mauaji mengi ya albino hutokea katika mazingira yanayoashiria kutokuwepo kwa usalama maalum kwa ajili ya maalbino.

Tunalishauri Jeshi la Polisi, likishirikiana na wadau mbalimbali nchini wakiwemo wananchi, lianzishe ulinzi maalum na endelevu kwa ajili ya maalbino, huku vyombo vingine vinavyohusika vikitimiza wajibu wa kutoa elimu dhidi ya wale wote wenye imani potofu kuhusu albino.

Mafanikio yoyote hupimwa kwa kuzingatia ni katika kipindi gani mafanikio hayo yamepatikana, kwa muda huu tulionao ni dhahiri kuwa ni mapema mno kwa Jeshi la Polisi kujisifia kuwa linapambana vema na wauaji wa albino"
.Nukuu hii inatokana na tahariri ya gazeti la Tanzania Daima la Desemba 2008

Kwa upande mwingine katika kubadili mtazamo wa jamii ikiwemo imani potofu juu ya jamii ya Albino nchini yapo baadhi ya mashirika ambayo yamekuwa yakijishughulisha na utoaji wa elimu

Moja kati ya Mashirika hayo ni Shirika la COEL- Tanzania lenye makao yake makuu mkoani Mwanza ambalo limekuwa likifanya kazi katika mikoa mbalimbali nchini, kwa kutoa elimu ya kuielimisha jamii namna ya kuondokana na imani potofu juu ya mauaji ya Albino na vikongwe.

Pamoja na mwenyekiti mtendaji wa shirika la COEL - TANZANIA kueleza kuwa wachimbaji wadogo ndiyo wamekuwa wakiminika kwa wanganga wa jadi (kienyeji), uchunguzi unaonyesha kuwa mtandao wa mauaji ya Albino ni mkubwa na unahitaji nguvu ya pamoja.

Ili kokumesha mauaji hayo kwanza ni kuhakikisha mtandao wa watu wote wanaojihusisha na mauaji hayo unathibitiwa kwa lengo la kuona jamii ya Albino inaendelea kuishi kama walivyo watu wengine na kupatamahitaji ya lazima.

Ni ukweli usiopingika kama mauaji hayo hayatatafutiwa njia mbadala ya kukomesha mauaji, jamii ya Albino itaendelea kuteketea hapa nchini na kuonyesha ni jinsin gani Tanzania inakiuka haki za binadamu licha ya kulithia makataba wa umoja wa mataifa ya haki za binadamu.

Kitendo cha jamii ya Albino kuendelea kuuawa ni moja kati ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa jamii hiyo ambayo kwayo inaonekana kutengwa kama si kusahaulika katika masuala ya haki za binadamu.

Kasi ya mauaji ya jamii ya Albino sikana kwamba yapo nchini bali hata nchi za jirani yameanza kujitokeza ikiwemo nchi ya Burundi.

Vyombo vya habari nchini vimekuwa mstari wa mbele katika kutoa habari za mauaji ya jamii ya Albino mara mauaji yanapotokea kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo makamanda wa polisi na viongozi wa maeneo husika.

Hata hivyo vita hivi si vya mtu mmoja au kundi furani bali nila jamii nzima kulingana na hali iliyopo hapa nchini na pia si jambo la kufumbia macho hata kidogo, kwani bila kufanya hivyo hatutaweza kuisaidia jamii hiyo ambayo inaonekana kukata tamaa

Kwa upande mwingine suala la kupewa simu kwa ajili ya kukabiliana na mauaji hayo siyo suluhisho kwa albino kutouawa kwani tangu tangazo hilo litolewe yapo baadhi ya mauaji ambayo yamekwishatokea.

Aidha jitihada zinazofanywa na mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali kuhamasisha jamii kuondokana na imani potofu juu ya mauaji ya albino bado kuna changamoto kubwa miongoni mwa jamii hiyo.

Kuamini kuwa viungo vya Albino vinaleta utajili ni imani potofu inayochangia mauaji hayo kutokana na waganga wa jadi hivyo, imani hiyo inayopaswa kulaaniwa kwani kila binadamu ana haki ya kuishi na si vinginevyo

Kutokana na wimbi la mauaji ya Albino nchini Serikali imeshaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha jamii ya Albino inaishi bila hofu na woga kama ilivyo kwa watu wengine.

Inasemekana kuwa zaidi ya Albino 25, wamekwisha uawa wakiwemo watoto wadogo ambao hawana hatia jambo linaonyesha kuwa ukatili dhidi ya watoto umekithidi nchini, licha ya kuwataka wauaji waache mara moja.

Ipo mikakati mingi dhidi ya Albino mojawapo ni ule wa Serikali kuamua kuwaweka katika kituo cha Mitindo kilichoko wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, ambapo zaidi ya Albino 100 wanaishi katika kituo hicho.

Pamoja na kuwaweka katika kituo hicho, bado kikakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa majengo,magodolo, vitanda pamoja na vifaaa kadhaa, pia suala la maji nalo limekuwa kero kwa watoto wanaoishi hapo.

Kero nyingine ni kukosekana kwa chakula cha kutosha kutokana na ongezeko la watoto waoishi katika kituo hicho hivyo ipo haja ya kutilia maanani suala hilo ambalo nalo nila muhimu kwa maisha ya watoto hao.

Katika kituo hicho wapo watoto wa kuanzia umri wa miaka mitatu na wazazi wa watoto hao wamekuwa hawana muda tena wa kwenda kuwaona kituoni hapa baada ya kuwapeleka na hata mahitaji kama vile sabuni, nguo na madawa hawawapelekei imekuwa ni mzigo mkubwa kwa uongozi wa kituo hicho.

Kutokana na changamoto zinazokikabili kituo hicho baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, watu binafsi, taasisi za dini na NGOS wamekuwa wakitoa msaada wa hali na mali.

Moja kati ya mashirika yaliyoweza kutoa msaada katika kituo hicho ni pamoja na shirika la Under the same sun lenye makao yake makuu nchini Canada kupitia kwa mkurugenzi wake mkazi Bw. Samwel Mluge.

Shirika la Under the same sun limeweza kutoa mashine za kutumia watu wasioona ambao ni miongoni mwa Albino walioko katika kituo hicho ambavyo ni moja kati ya changamoto linalokabili kituo hicho kutokana na upungufu wa vifaa.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Shirika lake litaendelea kukisaidia kituo hicho hata kama watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wataondoka katika kituo hicho, kurudishwa makwao kwani Albino walikoko kituo cha Mitindo wanatoka katika maeneo mbalimbali nchini

Anasema kuwa anatambua kwamba kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi lakini watatoa msaada kadri itakavyowezekana na ni moja kati ya majukumu ya Shirika lake kusaidiana na Serikali katika hilo.

Taarifa za changamoto kwa kituo hicho zimetolewa na mwalimu Zakayo Seleman wakati akisoma risala ya kituo mbele ya Mkurugenzi mkazi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Under the same sun Bw. Samwel Mluge.

Bw. Mluge alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa mashine kwa watoto wenye ulemavu wa macho( wasioona)katika kituo hicho, hafla ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.

Bw. Selemani anasema katika risala yake kuwa upo upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa,mabwenina madawati jambo linalochangia watoto hao waendelee kuhangaika katika kituo hicho.

Shirika la Under the same sun limekwishatoa misaada mingi katika kituo hicho kulingana na mahitaji halisi na uwezo walionao.

Zipo jitihada nyingi zinazofanywa na baadhi ya mashirika mbalimbali nchini kutoa elimu juu ya kuhakikisha mauaji ya Albino yanakomeshwa sanjari na kesi zilizoko mahakamani zinatolewa maamuzi ya haki.

Moja kati ya Mashirika hayo ni Shirika la COEL- Tanzania lenye makao yake makuu mkoani Mwanza ambalo limekuwa likifanya kazi katika mikoa mbalimbali nchini, kwa kutoa elimu ya kuielimisha jamii namna ya kuondokana na imani potofu juu ya mauaji ya Albino na vikongwe.

Pamoja na mwenyekiti mtendaji wa shirika la COEL - TANZANIA kueleza kuwa wachimbaji wadogo ndiyo wamekuwa wakiminika kwa wanganga wa jadi (kienyeji), uchunguzi unaonyesha kuwa mtandao wa mauaji ya Albino ni mkubwa.

Ili kokumesha mauaji hayo kwanza mi kuhakikisha mtandao wa watu wote wanaojihusisha na mauaji hayo unathibitiwa kwa lengo la kuona jamii ya Albino inaendelea kuishi kama walivyo watu wengine na kupatamahitaji ya lazima.

Ni ukweli usiopingika kama mauaji hayo hayatatafutiwa njia mbadala ya kukomesha mauaji, jamii ya Albino itaendelea kuteketea hapa nchini na kuonyesha ni jinsin gani Tanzania inakiuka haki za binadamu licha ya kulithia makataba wa umoja wa mataifa ya haki za binadamu.

Kitendo cha jamii ya Albino kuendelea kuuawa ni moja kati ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa jamii hiyo ambayo kwayo inaonekana kutengwa kama si kusahaulika katika masuala ya haki za binadamu.

Kasi ya mauaji ya jamii ya Albino si kana kwamba yapo nchini bali hata nchi za jirani yameanza kujitokeza ikiwemo nchi ya Burundi.

Vyombo vya habari nchini vimekuwa mstari wa mbele katika kutoa habari za mauaji ya jamii ya Albino mara mauaji yanapotokea kupitia kwa watu mbalimbali wakiwemo makamanda wa polisi na viongozi wa maeneo husika.

Hata hivyo vita hivi si vya mtu mmoja au kundi furani bali nila jamii nzima kulingana na hali iliyopo hapa nchini na pia si jambo la kufumbia macho hata kidogo, kwani bila kufanya hivyo hatutaweza kuisaidia jamii hiyo ambayo inaonekana kukata tamaa.

Akizungumzia mauaji ya jamii ya Albino hivi karibuni mwenyekiti wa chama cha Maalbino mkoa wa Mwanza Bw. Alfredy Kapole anasema kuwa haamini kama mauaji ya Albino nchini yameshindikana kukomeshwa.

Anasema kuwa kutokana na kuendelea kuuawa kwa Albino katika maeneo mengi nchini wameanza kukata tamaa ya kuishi na hasa ukizingatia walio wengi siku hizi hawafanyi kazi za kujitafutia fedha za kijikumu kwa madai kuogopa kuuawa.

Ameongeza kuwa katika awamu ya pili iliyokuwa ikiongozwa na Rais mstaafu Al Hassan Mwinyi, aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani wakati huo Bw. Augustin Lyatonga Mrema alikuwa mstari wa mbele katika kuwajibika ipaswavyo dhidi ya vita vya ujambazi na wanaotengeneza pombe haramu aina ya gongo.

Anasema katika kipindi hicho Bw. Mrema amewahi kuwataka wale wote wanaojihusisha na ujambazi kusalimisha silaha zao pia walewaliokuwa wakitengeneza pombe haramu aina ya gongo waliambiwa kusalimisha mitambo yao katika muda mfupi, jambo ambalo lilifanyika hivyo na kupata mafanikio makubwa katika mapambano hayo.

Hakuna siri kama Bw. Mrema aliweza kijizolea sifa nyingi katika kipindi hicho hasa kutoka kwa wale wanyonge ambao kwa kiasi furani waliteseka kutokana na ujambazi ambao ulikuwa umekithiri, licha ya wengine kuona kama biashara yao ilikuwa imeingiliwa.

Mwenyekiti huyo anahoji kwa nini katika serikali ya awamu ya nne waziri anayehusika asifanye kama waziri wa awamu ya pili alivyofanya kwa kutoa tamko kali dhidi ya wale wote wanaojihusisha na mauaji ya jamii ya Albino?

Ameongeza kuwa katika baadhi ya taarifa zinazotolewa na vyombo vingi vya habari zipo zile ambazo wapo watu wanokutwa na viungo vya jamii ya Albino, hivyo basi hakuna sababu ya kesi zao kucheleweshwa kusikilizwa mahakamani.

Anafafanunua kuwa hali hiyo ya uchelewashaji wa kusikiliza kesi hizo kunaleta hofu miongoni mwa jamii nzima siyo tu ile ya Albino kwa kuhisi kama kuna dalili ya mianya ya rushwa dhidi ya kesi hizo.

Aidha ameiomba serikali kuharakisha kusikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya Albino sanjari na kutoa maamuzi yaliyosahihi yasiyo na upendeleo wowote kwa maana ya kutaka haki itendeke.

Mwisho

No comments:

Post a Comment